YANGA SC INA UBORA NA SABABU ZA KUSHINDA TAJI LA 3 MFULULIZO VPL




Na Baraka Mbolembole

MECHI 6 za mzunguko wa pili ligi kuu Tanzania Bara 2016/17 zitapigwa Jumamosi hii, na nyingine mbili siku inayofuata ya Jumapili
.

Mabingwa mara mbili mfululizo na watetezi wa taji hilo, Yanga SC watafungua kampeni yao ya kusaka taji la tatu mfululizo dhidi ya African Lyon katika pambano ambalo watakuwa wenyeji katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam siku ya Jumapili.

YANGA ITASHINDA TAJI LA 3 MFULULIZO

Wana kikosi bora kilichozoeana ndani ya uwanja, wana wachapa kazi wa nguvu ambao wana uwezo wa kupambana hadi siku ya mwisho ya msimu katika kiwango kilekile huku wakipata matokeo. Hassan Kessy, Vicent Andrew, Juma Mahadhi, Beno Kakolanya, Mzambia, Obrey Chirwa ni maingizo mapya yaliyofanywa na kocha, Hans Van der Pluijm katika kikosi chake.

Mholland huyo amenyanyua tena kiwango cha kijana, Said Juma Makapu, na amekuwa katika jitihada za kuhakikisha, Malimi Busungu, Matheo Anthony wanarejea katika viwango vyao vilivyowafanya wakasajiliwa hapo mwaka mmoja uliopita. Wachezaji hawa nane niliowataja wanaweza kuisaidia Yanga msimu huu licha ya kwamba hawakuwa na msaada mkubwa katika msimu uliopita.

Busungu alikuwa katika changamoto ya kugombea nafasi na washambuliaji wa kimataifa, Mrundi, Amis Tambwe na Mzimbabwe, Donald Ngoma, bahati mbaya alisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara ila aliweza kufunga katika michezo muhimu dhidi ya Simba SC na Mtibwa Sugar katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro mwanzoni mwa msimu uliopita.

Matheo ambaye ‘alikubali’ kuonekana msaidizi wa Tambwe, Ngoma na Busungu lakini katika michezo kadhaa aliyopata nafasi akitokea benchi mshambulizi huyo alionesha kile alicho nacho.

Kama wachezaji wapya (Kessy, Andrew, Beno, Mahadh na Chirwa watafanya kazi inayotarajiwa na benchi la ufundi, Yanga itashinda taji la tatu mfululizo kwa maana kikosi chao chote cha kwanza kilichoshinda taji la 26 msimu uliopita kimebaki katika ubora wake.

Wengi wanatazama na kuchulia kushindwa kwa mabingwa hao wa Bara katika Caf Confederation Cup 2016 kama mojawapo ya sababu za kuamini kiwango cha timu hiyo kimeshuka. Kumbe sivyo.

Kwa jinsi nilivyowaona walinzi wa timu ya Ndanda FC walivyopata taabu kuwadhibiti washambuliaji wa kigeni wa timu ya Simba siku ya Jumamosi ya wiki iliyopita, ni dalili kwamba Ngoma ataendelea kuwatesa walinzi wa timu nyingine, watamchezea sana faulo ambazo zitawagharimu kadi na mikwaju ya penalti.

Tambwe ataendelea kuwa mfalme wa magoli ya kichwa. Zikiwa tayari zimechezwa game 7 (Yanga na JKT Ruvu hawajacheza) ni magoli 9 tu yamefungwa huku mechi ya Simba 3-1 Ndanda ikitoa magoli mengi zaidi katika michezo ya ufunguzi.

Inamaanisha beki ya Vicent Bossou/Andrew, Kelvin Yondan/Nadir Haroub, Juma Abdul/Kessy, Mwinyi Hajji/Oscar Joshua itakuwa ngumu kupitika na ili kufunga, Deo Dida/Ally Mustapha/Beno itahitaji washambuliaji makini wafungaji.

Yanga wana viungo wazuri, na uwepo wa Mnyarwanda, Haruna Niyonzima, Mzimbabwe, Thaban Kamusoko na vijana kama Deus Kaseke, Saimon Msuva, Mahadh, Geofrey Mwashuiya, Makapu na Mnyarwanda, Mbuyu Twite ina maanisha ubora wa timu hiyo unahitaji umoja, mshikamano, upendo na utulivu ndani hadi nje ya uwanja kama ilivyokuwa ndani ya miezi 24 iliyopita. Wachezaji watawalipa kwa taji la Taji la 3 mfululizo VPL.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top