Waasi nchini Colombia wasaini mkataba wa amani



Tamko la pamoja limesomwa katika sherehe zilizofanyika mji mkuu wa Cuba huko Havana

Serikali ya Colombia na kundi la waasi la Farc wamesaini mkataba wa amani kusitisha mgogoro uliopo zaidi ya miongo mitano. Wananchi wa Colombia wakifurahia baada ya makubaliano hayo

Pande zote mbili zimekubaliana kusaidia jamii, kuwapa haki zao waathirika wa mgogoro huo na kuleta amani.

Tamko la pamoja limesomwa katika sherehe zilizofanyika mji mkuu wa Cuba huko Havana,ambapo makubaliano hayo ya amani yalianzishwa karibu mika 4 iliyopita.

Mgogoro huo umesababisha vifo vya watu zaidi ya laki mbili na kuaawacha zaidi ya milioni bila ya makazi huko colombia.

Muda wa makubaliano wa mkataba huo bado unahitajika kuwekwa na wananchi wa Colombia kupitia kura ya pamoja itakayofanyika mwezi oktoba.
Farc wamekuwa wakipigana na serikali tokea mwaka 1964




Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top