VIDEO- LIVERPOOL YAUA NA KUTINGA RAUNDI YA TATU EFL


Liverpool iliyosheheni nyota wake wote usiku wa kuamkia leo imefanya kufuru baada ya kutoa kipigo kitakatifu cha mabao 5-0 dhidi ya timu ya Ligi Daraja la Kwanza Burton Albion na kutinga raundi ya tatu ya Kombe la EFL
.

Iliwachukua dakika 15 tu Liverpool kupata bao la kwanza kupitia kwa Divock Origi baada ya kuusindikiza mpira wavuni, kabla ya Roberto Firmino kuongeza lingine baada ya kuunganisha krosi nzuri iliyochongwa na Nathaniel Clyne na kufanya matokeo kuwa 2-0.

Origi alitaka tena kuongeza lingine baadaye lakini mpira uliokolewa na kipa wa Burton Albion Stephen Bywater.

Tom Naylor alijifunga mwenyewe na kuipatia Liverpool bao la tatu dakika ya 61, kabla ya Daniel Sturridge ambaye aliingia kutokea benchi kufunga mawili mnamo dakika ya 78 na 83 na kuhitimisha karamu ya mabao 5-0 kwa Liverpool.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top