Mkwasa atangaza kikosi cha wachezaji 20 kuikabili Nigeria, Ulimwengu nje


Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Charles Boniface Mkwasa ameita kikosi cha wachezaji 20 kwa ajili ya mchezo wa kukamilisha ratiba kuwania kufuzu kombe la dunia dhidi ya Nigeria.

Mechi hiyo itachezwa September 3 mwaka huu nchini Nigeria, huku timu zote (Nigeria na Tanzania) zikiwa tayari zimeondoshwa kwenye mashindano kutoka Kundi G.

Wachezaji walioitwa ni pamoja na;

Magolikipa: Deogratius Munishi ‘Dida’ (Yanga SC) na Aishi Manula (Azam FC)

Walinzi: Kelvin Yondani, Mwinyi Haji, Vicent Andrew ‘Dante’ (Yanga SC), David Mwantika, Shomari Kapombe (Azam FC) na Mohamed Hussein (Simba SC).

Viungo: Himid Mao (Azam FC) Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Jamal Mnyate Mudhamiru Yassin (Simba SC), Ibrahim Rajab ‘Jebba’ (Tibwa Sugar) na Juma Mahadh na Simon Msuva (Yanga).

Washambuliaji: John Bocco, Farid Musa (Azam FC), Ibrahim Ajib (Simba SC) na Mbwana Samatta (KRC Genk).

Wachezaji walioitwa Stars wanatakiwa kuripoti kambini Agosti 28, huku mazoezi yakitarajiwa kuanza Agosti 29 kabla ya kusafiri kuelekea Nigeria kwa ajili ya mchezo huo.

Mkwasa amesema amemuacha Thomas Ulimwengu anaecheza TP Mazembe kutokana na mshambuliaji huyo kuwa majeruhi (goti) kwa takribani wiki tatu na hajaonekana kuitumikia klabu yake katika mechi za hivi karibuni.

Ameongeza kuwa, wachezaji wengi walioitwa kwenye kikosi hicho ni vijana kwa ajili ya kuwapa uzoefu huku wakongwe kadhaa wakiwepo kwa ajili ya kuwaongezea kujiamini vijana walioitwa.
 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top