TP MAZEMBE YAICHAPA YANGA TENA NA KUONGOZA KUNDI A


Mchezo wa mwisho wa Kundi A michuano ya kombe la Shirikisho Afrika kati ya TP Mazembe dhidi ya Yanga umemalizika kwa Yanga kukubali kichapo cha magoli 3-1 ikiwa ugenini na kuendeleza
rekodi yake ya kutoshinda michezo yake mitatu ya hatua ya nane bora msimu huu.
Bolingi alianza kuifungia Mazembe bao la kwanza dakika ya 28 kipindi cha kwanza.
MZ 4
Yanga ilipata pigo dakika mbili baada ya kuruhusu goli, Andrew Vicent ‘Dante’ alioneshwa kadi nyekundu na kuiacha Yanga ikicheza pungufu kwa dakika zote zilizobaki.
MZ 2
Dakika 11 baada ya kipindi cha pili kuanza, Rainford Kalaba aliifungia Mazembe bao la pili kabla kuongeza bao lake la pili likiwa ni bao la tatu kwa Mazembe mnamo dakika ya 64.
Amis Tambe aliifungia Yanga bao pekee akiunganisha mpira uliogonga ‘mtambaa panya’ baada ya Haruna Niyonzima kupiga mpira wa adhabu ndogo.
MZ 5
Matokeo hayo yanaipa Mazembe fursa ya kuongoza Kundi A kwa pointi 13 bila kujali matokeo ya wapinzani wake Medeama na MO Bejaia.Kikosi cha Yanga kilichopambana na TP Mazembe leo bofya hapa




Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top