RC Makonda: Polisi Mkikuta Mtu Yeyote Msituni Pigeni bila Huruma, Haki za binadamu Wakiwauliza Waambieni waje Kwangu

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameliagiza Jeshi la Polisi kuwagonga na kuwapiga wahalifu wowote wakiwamo majambazi pindi wanapowakamata


Akizungumza wakati wa kuaga miili ya askari watatu kati ya wanne wa Jeshi la Polisi waliouawa wiki hii katika tawi la benki ya CRDB lililopo Mbande wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, Makonda alisema jambazi atakapokutwa popote iwe msituni iwe wapi agongwe na apigwe. 


Alisema alipopata taarifa ya vifo vya askari hao wanne alifungua pazia za madirisha nyumbani kwake na kuwaangalia askari wanaolinda na kulia kwa uchungu na kwamba usiendelezwe ukichaa wa haki za binadamu kwani ni uendawazimu ambao hauwezi kuvumilika. 


“Kamanda Sirro (Simon) mimi ndiyo mkuu wako wa mkoa nasema ukikamata hao watu popote gonga, piga na watu wa haki za binadamu wakija waambie waje kwangu, hatuwezi kukaa kwenye mkoa ambao haupo salama,” alisema Makonda aliyedai hana maneno mazuri ya kusema kwa sababu hakuumbwa kumfurahisha mtu, bali anafanya kazi ya Mungu na wakati wake ukiisha ataondoka.


“Kama kuna haki za binadamu nataka haki za askari wangu kwanza. Kama hao watu wa haki za binadamu wapo nataka kuona wakiandamana kukilaani kitendo hiki, ”alisema Makonda.


Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top