Rais wa zamani wa FIFA afariki dunia

Mashindano sita ya kombe la dunia yalifanyika chini ya utawala wake
Rais wa zamani wa FIFA Joao Havelange amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 100.Mbrazil huyo alikuwa mtangulizi wa Sepp Blatter katika shirikisho la mpira wa miguu duniani kuanzia mwaka 1974 hadi 1998
.

Alijiuzulu nafasi ya Urais wa FIFA April 2013 kufuatia uchunguzi wa madai ya kupokea rushwa,na kulazwa

hospitalini mwaka uliofuata alipokumbwa na ugonjwa wa mapafu.

Alikuwa mmoja wa wanakamati wa Olympic (IOC), kuanzia mwaka 1963 hadi 2011 alipojiuzulu kwa sababu ya kudhoofu kwa afya yake.

Havelange aliiwakilisha Brazil katika mashindano ya Olympic ya Kuogelea mwaka 1936,mwaka ambao aliidhinishwa kuwa mwanasheria kabla ya kuchaguliwa na IOC.

Akiwa kiongozi wa FIFA aliongeza washiriki wa kombe la dunia kutoka timu 16 hadi 32, ambapo mashindano 6 yalifanyika chini ya utawala wake.
 Habari za Magazetiya Leo Jumanne August 16, 2016 bofya hapa

MANJI AJIUZULU YANGA bofya hapa







Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top