Rais wa zamani Kenya Mwai Kibaki alazwa Afrika Kusini

Bw Kibaki aliongoza Kenya kati ya 2002 na 2013

Aliyekuwa Rais wa Kenya Mwai Kibaki, 84, amelazwa hospitalini nchini Afrika Kusini akipokea matibabu maalum baada ya kuugua mwishoni mwa wiki.

Kiongozi huyo wa zamani aliugua akiwa nyumbani kwake na akapelekwa hospitalini Karen, Nairobi Jumamosi jioni kabla ya kusafirishwa Afrika Kusini Jumapili.

"Aliandamana na daktari wake. Tunamtarajia arejee nyumbani hivi karibuni, na Wakenya watafahamishwa kuhusu hali yake wakati mwafaka," taarifa iliyotolewa na familia yake ilisema.

Desemba mwaka 2002, Bw Kibaki aliumia baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani wakati wa kampeni na akapelekwa Uingereza kwa matibabu.

Aliapishwa kuwa rais muhula wake wa kwanza akiwa kwenye kiti cha magurudumu.Bw Kibaki na mkewe Lucy

Mkewe, Lucy Muthoni Kibaki, alifariki Aprili mwaka huu akitibiwa jijini London.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top