Mfalme Akihito wa Japan aomba kung’atuka

Wananchi waonekana kushangaa baada ya Mfalme Akihito kutangaza matamanio yake ya kung'atuka

Mfalme wa Japan Akihito ameeleza mapenzi yake ya kutaka kung'atuka.

Akihutubia taifa hilo kupitia runinga, amesema ana wasiwasi kwamba umri na udhoofu wa afya yake huenda vikamfanya ashindwe kutekeleza majukumu yake.

Kwa sasa, hakuna nafasi kisheria kumruhusu mfalme kuondoka madarakani Japan.

Lakini muda mfupi baada ya hotuba yake, Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe, amesema atathmini kwa makini matamanio ya mfalme huyo. Mfalme Akihito

Mfalme Akihito amekuwa madarakani tangu kifo cha babake, Hirohito, mwaka 1989.

Habari kwamba anataka kung'atuka zilianza kutokea kwenye vyombo vya habari mwezi jana.
 
 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top