Zuma asubiri uamuzi kuhusu mashtaka

Baadhi ya mashtaka yanahusu mkataba wa ununuzi wa silaha

Waendesha mashtaka mkuu nchini Afrika Kusini wanatarajiwa kufichua leo iwapo watafufua mamia ya<endelea bofya kichwa cha habari hii juu> mashtaka ya ulaji rushwa dhidi ya Rais Jacob Zuma au la.

Hii ni kufuatia uamuzi wa mahakama mwezi jana ambayo ilisema uamuzi wa kutupilia mbali mashtaka hayo haukuwa wa busara na unafaa kutafakariwa upya.

Mashtaka hayo yanajumuisha kashfa kubwa ya mabilioni ya dola ya ununuzi wa silaha iliyofutiliwa mbali mwaka 2009.Zuma amekabiliwa na shinikizo za kumtaka ajiuzulu

Kufutiliwa mbali kwa mashtaka hayo kulimfungulia njia Bw Zuma kushinda urais wiki chache baadaye.

Wachanganuzi wa masuala ya kisiasa wanasema iwapo mashtaka hayo yatafufuliwa, basi hatua hiyo itaongoeza shinikizo za kumtaka Bw Zuma ajiuzulu.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top