Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad anatarajiwa kurejea leo kutoka ughaibuni alikoenda kwa ziara ya takribani wiki tatu huku jeshi la polisi likijiandaa kumfikisha
Mahakamani.
Mahakamani.
Hivi karibuni, Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu alieleza kuwa Jarida la Mashtaka dhidi ya Maalim Seif liko kwa Mkurugenzi wa Mashtaka wa Zanzibar, kutokana na kile alichodai kuwa aliwachochea wafuasi wake kufanya fujo kupitia vikao vya ndani vya chama hicho.
IGP Mangu alieleza kuwa uchaguzi wa Oktoba 25 na ule wa Marudio vilifanyika kwa amani na utulivu lakini matatizo na vitendo vya uvunjifu wa amani vilianza kuonekana tangu mwanasiasa huyo aliyegombea Urais kuanza kufanya mikutano hiyo ya ndani akiwahamasisha wafuasi wake kutoshirikiana na Serikali iliyopo madarakani.
Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Makame amethibitisha kuwa tayari jalada hilo liko kwa DPP na kwamba upelelezi unaendelea.
Akizungumzia mpango huo wa Jeshi la Polisi, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa CUF, Shemeji Mketo aliwaambia waandishi wa habari kuwa chama hicho kimekuwa kikisubiri polisi watekeleze azimio lao hilo ndipo wataeleza msimamo wao.
“Acha wamkamate na sisi tunalisubiri hilo… wakimkamata ndipo tutasema nini tunafanya,” alisema Mketo.
Aidha, Mketo alisema kuwa Maalim Seif atakapowasili atazungumza na waandishi wa habari kuelezea kuhusu ziara yake, nchi alizokwenda na mambo aliyoyafanya.
Vyama 9 Vya Siasa Kufutwa bofya hapa
Polisi Wamnyima Tundu Lissu Dhamana, Atupwa Rumande bofya hapa
Video:Sababu ya Rais wa Simba kukamatwa na TAKUKURU hii hapa bofya hapa
Habari Zilizopo katika Magazeti ya Leo Ijumaa August 05, 2016 bofya hapa
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)