BACCA AANZA NA HAT-TRICK SERIE A


Mshabuliaji Carlos Bacca amefunga hat-trick kwenye mechi ya kwanza ya AC Milan katika ufunguzi wa msimu mpya wa Serie A dhidi ya Torino.

Nyota huyo mwenye miaka 29 aliyehusishwa kujiunga na West Ham, aliifungia Milan bao la kwanza kwa kichwa kabla ya mapumziko kabla ya Andrea Belotti kusawazisha.

Bacca akafunga bao jingine kisha kumalizia hat-trick yake ya kwanza ndani ya Serie A kwa mkwaju wa penati.

Daniele Baselli akaifungia Torino bao dakika za majeruhi dakika chache kabla ya golikipa wa Ac Milan Gianluigi Donnarumma kupangua penati ya Belotti dakika za lala salama baada ya Gabriel Paletta kuzawadiwa kadi nyekundu kutokana na mchezo mbaya.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top