Abiria wa kike kutengwa na wanaume ndani ya Feri



Abiria wakiingia katika Feri ya Likoni huko Mombasa Kenya

Baraza la kaunti ya Mombasa nchini Kenya linapanga kuwatenga abiria wa kiume na wenzao wa kike katika kivuko cha likoni kufuatia visa vya unyanyasaji
wa kingono katika kivuko hicho.

Baraza hilo tayari limezindua mpango huo kufuatia mapendekezo ambayo yameungwa mkono na serikali kuu pamoja na ile ya baraza hilo.

Tayari serikali ya Kenya imelipatia shirika la huduma za ferry katika kivuko hicho shilingi milioni 250 ili kuweka kamera za kuwachunguza wanaume hao wanaowanyanyasa wanawake pamoja na wahalifu wengine wanaoabiri feri hiyo.

Madiwani wa eneo hilo walichukua hatua hiyo kufuatia malalamishi kwamba wanawake huviziwa na baadaye kunyanyaswa kingono wakati feri hizo zinapojaa watu.

Wanaume kadhaa wamepatikana na hatia na kufungwa jela kwa kuwavizia na kuwashika abiria wawanawake.

Mtu mmoja anahudumia kifungo jela baada ya kupataikana na hatia ya kumnyanyasa mwanamke katika kivuko hicho.

Katika kisa chengine ,mtu mmoja alipigwa na abiria alipojaribu kumpiga busu mwanamke ndani ya feri hiyo.

Polisi Wamnyima Tundu Lissu Dhamana, Atupwa Rumande bofya hapa

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top