
Premier Legue iliwakilishwa na wachezaji wengi kwenye michuano ya Euro 2016 huko Ufaransa lakini katika hatua ya fainali wamesalia wachezaji 12 pekee kutoka kwenye ligi hiyo yenye watazamaji lukuki duniani. Yamebaki mataifa mawili hadi sasa ambayo yatacheza fainali ya Euro 2016, wenyeji Ufaransa ambao walifika hatua ya fainali siku ya Alhamisi usiku baada ya ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya washindi wa Kombe la Dunia Ujerumani, watakabiliana na Ureno siku ya Jumapili usiku.
Vilabu nane vya Premier League vitawakilishwa na wachezaji wao kwenye hatua hii huku Manchester United na wapinzani wao wa karibu Manchester City wakiwakilishwa na wachezaji wao wawili kama ilivyo kwa Arsenal pia.
Kuna utitiri wa wachezaji wa Premier League kwenye kikosi cha Ufaransa wakati huo ukimtoa kiungo wa Newcastle Moussa Sissoko ambaye timu yake imeshuka daraja mwishoni mwa msimu uliopita 2015/16 na itacheza Championship.
Kukiwa na wachezaji 12 wa Premier League, 10 kati yao wanacheza kwenye timu ya taifa ya Ufaransa wakati wawili wanaiwakilisha Southampton watakuwa wakiitetea Ureno.
Hapa kuna list ya wachezaji wa Premier League waliotinga fainali ya Euro 2016:
Ureno:
Jose Fonte-Southampton

Cedric Soares-Southampton

Ufaransa:
Hugo Lloris-Tottenham Hotspur

N’Golo Kante-Leicester City

Yohan Cabaye-Crystal Palace

Dimitri Payet-West Ham United

Olivier Giroud-Arsenal

Anthony Martial-Manchester United

Morgan Schneiderlin-Manchester United

Eliaquim Mangala-Manchester City

Bacary Sagna-Manchester City

Laurent Koscielny-Arsenal

Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)