MATERAZZI AMEONGEA KWA MARA YA KWANZA ILE ISHU YA KUPIGWA KICHWA NA ZIDANE


Marco Materazzi kwa mara ya kwanza ametanabaisha kile alimwambia Zinedine Zidane kabla ya kupigwa kichwa kwenye fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2006. Vile vile amekiri kwamba tukio lile lilibadilisha kabisa mfumo wa maisha yake baada ya kuanza kufuatiliwa kwa karibu sana vyombo vya habari.

“Tangu siku ile, nilianza kuombwa kufanya mahojiano na vyombo mbalimbali duniani. ” Materazzi aliongea na L’Equipe (kupitia gazeti la Marca).

“Niliamua kuchapisha kitabu juu ya tukio lile kwa sababu kila mtu alikuwa akiniuliza ni kitu gani hasa nilimwambia Zidane kiasi cha kufikia hatua ya kufanya tukio lile. Maneno hayakuwa mazuri lakini hata hivyo sikupaswa kuhukumiwa kwa namna ile. Kwenye maeneo mengi ninayoyafahamu kama Rome, Naples, Turin, Milan Paris, huwa nasikiga zaidi hata ya nilichomwambia, ” aliongeza.

“Mimi nilimzungumzia dada yake na wala sio mama yake, kama ambavyo nimesoma kwenye baadhi ya magazeti. Mama yangu alikufa nikiwa kijana mdogo sana, hivyo isingekuwa rahisi kwangu kutukana tusi hilo.”

Marco Materazzi alienda mbali zaidi na kusema kwamba haelewi kwanini stori ile ilipaishwa sana na vyombo vya habari namna ile.

“Sijui kwanini stori ile iliwekwa chumvi kiasi kile. Kitu pekee ambacho naweza kukumbuka kutoka kwenye fainali ile ni magoli yangu mawili niliyofunga.”

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top