Video:Waziri Mkuu Mhe Majaliwa atamka rasmi kuhamia Dodoma na kuagiza mawaziri wote wamfuate


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe: Kassim Majaliwa, akiwa katika sherehe ya Kumbukumbu ya Siku ya Mashujaaa amesema atahamia Dodoma ifikapo mwezi wa 9 mwaka huu na kuwataka mawaziri wote wamfuate
.


Aagiza ukarabati wa nyumba yake iliyopo Dodoma uanze mara moja.

Uamuzi huu wa Waziri Mkuu unaakisi makusudio ya Rais Magufuli kuhamishia shughuli zote za serikali katika Mji Mkuu wa nchi Dodoma kufikia 2020.

Rais Magufuli aliahidi katika kipindi cha uongozi wake Serikali yote itahamia Dodoma.

Juzi katika mkutano wa CCM, Rais Magufuli alikumbushia ahadi hiyo ya kuhamia Dodoma na kusema kuwa kabla hajamaliza miaka yake 5 Serikali yote itakuwa mjini Dodoma.






Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top