Breaking news:Mahakama kuu kanda ya Iringa imemtia hatiani kwa kuua bila kukusudia Askari aliyehusika na mauaji ya Mwangosi

Mahakama Kuu Kanda ya Iringa Leo Jumatatu July 25, 2016, Imemtia hatiani kwa kuua bila kukusudia askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Iringa (FFU), Pasificus Simon, aliyehusika na

mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa Channel Ten na mwenyekiti wa Iringa Press Club marehemu Daud Mwangosi huku ikiahirisha kutoa adhabu mpaka tar.27 juma tano hii ili kupitia mapendekezo ya adhabu yaliyotolewa na upande wa jamhuri uliotaka afungwe maisha na maombi ya kupunguza adhabu kwa mshitakiwa yaliyotolewa na wakili wa upande wa utetezi,Kesi ipo chini ya jaji Dk.Paul Kihwelo.

Ikumbukwe Mwangosi aliuawa kwa kupigwa bomu Septemba 2, 2012 katika Kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi alipokuwa akiwajibika kwa kazi za kihabari wakati wa ufunguzi wa matawi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Habari zaidi endelea kufuatilia uchambuzileo 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top