Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), itaanza kudahili wanafunzi waliomaliza kidato cha sita wanaoomba kujiunga na vyuo vikuu kuanzia Leo
.
.
Akizungumza juzi, Kaimu Mkurugenzi wa Udahili na Nyaraka wa TCU, Dk Kokubelwa Mollel alisema udahili kwa wenye diploma utaanza Julai 31.
Dk Mollel alisema kazi hiyo itaendelea kwa mwezi mzima ili kuruhusu wananchi wengi zaidi kupata fursa ya kuomba kudahiliwa na udahili huo utafanyika kwa njia ya mtandao.
Alisema ili wanafunzi waweze kuelewa programu zinazotolewa na vyuo vikuu, tume hiyo imeandaa maonyesho ya 11 yatakayofanyika kuanzia Julai 20 hadi 22, mwaka huu.
Alisema maonyesho hayo yatafanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kufunguliwa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako.
Breaking News!! Kiwanda cha Polister kinaungua moto Kihonda Morogoro bofya hapa
Breaking news:Wakurugenzi sita wasimamishwa kazi NSSF Bofya hapa
Breaking news:Wakurugenzi sita wasimamishwa kazi NSSF Bofya hapa
Matokeo ya form six 2016 bofya hapa
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)