PELLE KAINGIA KWENYE LIST YA RONALDO NA MESSI YA KULIPWA MKWANJA MREFU ZAIDI


Kwanini Graziano Pelle ameenda Shandong Luneng?

Baada ya wiki kadhaa za tetesi, sasa ni rasmi kwamba mshambuliaji wa Italy Graziano Pelle ameejiunga rasmi na klabu ya Shandong Luneng ya nchini China.
(Ronaldo ampiku Messi bofya hapa)
Huu ni usajili mwingine wa pesa nyingi kwa mastaa wanaelekea nchini China baada ya ule wa Mbrazil Hulk. Pelle ataungana na mchezaji wa zamani wa Newcastle Papiss Cisse kunako klabu hiyo ya Shandong Luneng.

Watu wengi wamekuwa wakijiuliza kwanini Pelle ameamua kujiunga na Shandong Luneng wakati bado yuko kwenye ubora waa hali ya juu hasa ukizingatia kwamba ametoka kufanya mambo makubwa kwenye michuano ya Euro iliyomalizika hivi karibuni na kuisaidia klabu yake za zamani ya Southampton kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Europa msimu ujao.

Atakuwa akilipwa euro 350, 000 kwa wiki.

Hii ndiyo sababu kubwa ya Pelle kuelekea nchini China. Atakuwa akilipwa mpunga mkubwa mno, ambapo kwa umri wake wa miaka 30 ni wakati sahihi mno kwake kwenda kuvuna kiasi kikubwa kama hicho.

Inaweza kuchukuliwa kama ameenda kujitopeza katika ramani ya soka, lakini kwa sasa Pelle atakuwa mchezaji wa sita duniani kulipwa mshahara mkubwa zaidi katika ulimwengu wa soka.

Ni Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Hulk, Neymar na Zlatan Ibrahimovic pekee kwa sasa ndio wanamzidi kwa kulipwa vizuri zaidi.

Atakuwa alikilipwa euro 50 000 kwa siku.

Muitaliano huyo kwa sasa atakuwa akipata euro milioni 2.5 kwa mwaka, pesa nyingi zaidi ya mshambuliaji wa Bayern Munich na Ujerumani Thomas Muller.

Wanaoongozwa kwa kulipwa pesa nyingi zaidi kwa mwaka

1 CR7 – euro milioni 21

2 Messi euro milioni 20

3 Hulk -euro milioni 20

4 Neymar-euro milioni 19

5 Ibra- euro milioni 16

6 Pellé-euro milioni 16

7 TMüller-euro milioni 13.5

8 Lavezzi-euro milioni 13

9 JacksonM. 12.5

10 TSilva 12



 
 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top