Jeshi La Polisi Lakamata Vipande Vya Meno Ya Tembo 666 Vyenye Thamani Ya Zaidi Ya Sh.bilioni Nne.


JESHI la Polisi nchini kwa kishirikiana na Ofisi za Interpol Kanda ya Kusini Mwa Afrika imefanya operesheni na kukamata vipande vya meno ya Tembo 666 vyenye uzito wa Kilogram 1279.19 vyenye thamani zaidi ya Sh. Biloni Nne.


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kamishna wa Jeshi la Polisi (CP), Diwani Athuman wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.Amesema kuwa vipande hivyo vya tembo vimehusisha watu tisa kati yao mmoja ni Raia wa Guinea na mwingine ni Raia wa Uganda.


Amesema kuwa katika operesheni Usalama III wameweza kukamata vitu mbalimbali kutokana na taarifa za kiitelijensia zilizokusanywa wakati wa matayarisho ya operesheni ya Usalama III, ambapo waliweza kukamata mitambo 18 ya kutengenezea gongo pamoja na lita za gongo 960 zimekamatwa.


Athuman amesema katika Operesheni hiyo wameweza kukamata watuhumiwa 265 ambapo baada ya uchunguzi watakaobainika kuhusika na vitendo vya kihalifu watafikishwa mahakamani mara moja


Kamishina Othman amesema ametoa rai kwa wanunuzi wa magari nje ya nchi kuwasiliana na ofisi za Interpol za ndani au nje ya nchi magari yanakotoka kwa uchunguzi kabla ya kuyanunua ili kuondoa usumbufu wa kukamatwa mara kwa mara katika operesheni kama hizi.


Amesema kutokana na operesheni hiyo jeshi la polisi halitakubali kuona kundi la watu wachache linalotishia usalama wa maisha ya raia wema na mali zao na wataobainika kufanya hivyo watachukuliwa hatua za kisheria bila kusita.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top