Breaking news: Koffi Olomide Ahukumiwa Jela

Koffi Olomide wakati akikamatwa na polisi  mjini Kinshasa.

Mwanamuziki nguli wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Koffi Olomide amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela huko DRC kwa kumpiga teke mmoja wa madansa wake aitwaye Pamela akiwa nchini Kenya.

Nguli huyo wa muziki wa Rhumba amehukumiwa muda mfupi baada ya kukamatwa na polisi akiwa nyumbani kwake mjini Kinshasa leo.



Koffi alikana tuhuma za kumpiga dansa huyo na mwanasheria wake aitwaye George Wajackoyah naye amelaani kitendo cha polisi kutumia nguvu kubwa wakati wa kumkamata staa huyo.
VIDEO: Koffi Olomide adaiwa kumpiga teke mwanamke Kenya bofya hapa
Staa huyo alikamatwa nchini Kenya Ijumaa iliyopita na kurudishwa DRC kesho yake asubuhi baada ya video yake kusambaa mitandaoni ikimuonesha akimpiga teke mmoja wa madansa wake aitwaye Pamela mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Jomo Kenyatta (JKIA) kwa ajili ya tamasha.

Koffi anadaiwa kufanya tukio hilo baada ya Pamela kukorofishana na mwanamuziki wake aitwaye Cindy Le Couer anayedaiwa kuwa ni mpenzi wa Koffi.
 
 Breaking news: Ajali mbaya ya Basi la UDA lagonga Treni Kariakoo,Mmoja Afariki, 45 Wajeruhiwa bofya hapa
 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano July 27, 2016 bofya hapaNAFASI  ZA KAZI BOFYA HAPA 



Tume ya vyuo Vikuu Tanzania( TCU) yatangaza vyuo Vikuu vilivyofungiwa BOFYA HAPA


News alet:Majina ya wanafunzi waliochanguliwa kujiunga Certificate na Diploma na NACTE 2016/2017 bofya hapa

News alert:Tume ya vyuo Vikuu Tanzania( TCU) yatangaza vyuo Vikuu vilivyofungiwa BOFYA HAPA
 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top