Breaking news: Ajali mbaya ya Basi la UDA lagonga Treni Kariakoo,Mmoja Afariki, 45 Wajeruhiwa


Basi la UDA lenye namba za usajili T 696 CVP limegonga treni katika eneo la Kamata Jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo wakati Basi hilo likitokea stendi ya Gerezani Kariakoo kuelekea Mbagala
na kuua mtu mmoja na wengine zaidi ya 45 kujeruhiwa.
 
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Ernest Matiku amesema majeruhi wamepelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu.
 
Hata hivyo, hakuweza kumtaja jina mtu huyo aliyefariki dunia.


“Ni kweli ajali imetokea kuna kifo cha mtu mmoja na watu wengi wameumia sana ,” amesema Kaimu kamanda huyo.






Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top