YANGA SC yashindwa kutamba nyumbani katika michuano ya CAF Confederation Cup.
Mchezo huo uliopigwa katika dimba la
uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Jumanne hii. TP Mazembe wametoka na ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Yanga goli lililofungwa dakika ya 75
Hivi ndivyo hali halisi ilivyokuwa uwanja wa Taifa, soma uchambuzi huu juu ya ushiriki wa Yanga katika michuano hii
Bado Yanga wanaendelea kuusaka ushindi wao wa kwanza kwenye hatua ya makundi ya kombe la shirikisho Afrika.
Baada ya kupoteza mechi yao kwanza ugenini dhidi ya MO Bejaia ya Algeria, leo walikuwa nyumbani wakikipiga dhidi ya TP Mazembe mchezo uliomalizika kwa Yanga kupoteza tena kwa goli 1-0.
Goli la Mazembe lilitokana na mpira wa adhabu ndogo baada ya Kelvin Yondani kumuangusha Thomas Ulimwengu nje kidogo ya eneo la hatari. Mpira wa adhabu ndogo ulimfikia Merveille Bope na kuupachika kambani baada ya mabeki wa Yanga kushindwa kuuondosha kwenye eneo lao la hatari.
Yanga-mechi 2 bila goli
Tayari Yanga imeshacheza mechi mbili kwenye hatua ya makundi, wamefungwa zote kwa goli moja (kila mechi) huku wao wakiwa bado hawajafunga bao hata moja katika mechi walizocheza.
Chirwa, Mahadhi, mambo poa
Nyota hawa wa Yanga walikuwa wanacheza mechi yao kwa mara ya kwanza wakiwa Yanga huku Mahadhi akicheza mechi ya kwanza ya kimataifa.
Wote kwa pamoja wameonesha uwezo mkubwa kwa muda waliopata nasi ya kucheza. Mahadhi aliumia na kushindwa kuendelea na mchezo na nafasi yake kuchukuliwa na Geofrey Mwashiuya huku Obrey Chirwa yeye nafasi yake ilichukuliwa na Matheo Athony.
Uingereza yatolewa michuano ya EURO 2016 Bofya hapa
Video: MESSI AKOSA PENATI NA KUISHUHUDIA CHILE IKITWAA UBINGWA COPA AMERICA bofya hapa
Breaking news: Rais Magufuli ateua Wakuu wa Wilaya na kufanya mabadiliko kidogo ya wakuu wa mikoa bofya hapa
Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA
HABARI KUU LEO BOFYA HAPA