YANGA KUKWEA PIPA USIKU WA MANANE.

Kikosi cha timu ya Yanga.
KUNDI la kwanza la wachezaji wa Yanga wanatarajiwa kuondoka usiku wa leo kuelekea nchini Uturuki kwa ajili ya kuweka kambi maalumu ya kujiandaa na mchezo wao wa kwanza wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Mo bejala ya Nchini Algeria utakaopigwa kati ya Juni 17,18,19. Hatua hiyo imekuja baada ya uongozi wa Yanga kukosa ndege ya pamoja na kuamua kiwasafirisha wachezaji wake kwa makundi mawili huku wengine wakitarajiwa kuondoka kesho sa 10 jioni.


Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano Yanga, Jerry Muro amesema kuwa wachezaji watakaosafiri jumla ni 21 ikijumuishwa na benchi la ufundi saba pia wataongozana na mjumbe wa kamati ya utendaji mmoja kwani timu inakwenda kwa ajili ya kujiandaa na hawatataka wapate usumbufu wa aina yoyote ndiyo maana wameonelea benchi la ufundi lifanye kazi yake kwa ufasaha. Uamuzi huo umekuja zaidi kwa ajili ya kubana matumizi ila viongozi wengine wataondoka Juni 15 kuanzia hapa kuelekea nchink Algeria kwa ajili ya kuungana na wachezaji.


"Wachezaji wataondoka kwa awamu mbili, leo saa nane usiku na wengine kesho saa kumi jioni ila wataongozana na kiongozi mmoja wa kamati ya utendaji pamoja na saba kutoka benchi la ufundi, "amesema Muro. Hata hivyo kikosi kitakaa kwa muda hadi Juni 15, ambapo wataanza safari ya kwenda nchini Algeria ila mpaka leo bado hawajajua mechi itakuwa lini kati ya tarehe zilizokuwa zimepangwa na Shirikisho la Soka Afrika CAF ila hata kama ikiwa Juni 17, kikosi kitakuwa kamili kuvaana nao.


Yanga itawakosa Juma Abdul ambaye ni majeruhi na Nahodha Nadir Haroub 'Canavaro' anayetumikia kadi nyekundu aliyoipata kwenye mchezo wao wa hatua ya 16 bora dhidi ya Segrada Esperanca ya nchini Angola ambayo itamuweka nje kwa mchezo mmoja.
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top