WEKA KANDO TABIA ZA DJEMBA DJEMBA NA WENZAKE, HUYU BAILLY NI FORTUNE MWINGINE

Wakati mwingine tunasoma au kusimuliwa historia kuhusu matukio yaliyotokea zamani. Binafsi sikuwahi kumshuhudia Fortune akicheza lakini alikuwa na
sifa za kipekee ambazo nimekuwa nasimuliwa na wale waliowahi kumuona. Naambiwa alikuwa na nidhamu pia alipenda kuchomekea jezi yake kama mwanafunzi mnatashati. Fortune alikuwa anatoka Afrika Kusini.

Katika historia niliyosimuliwa kuhusu Fortune najaribu kuwaza kuhusu Eric Djemba Djemba ambaye nami nitawasimuliwa ambao hawakuwahi kumuona. Djemba Djemba ni tofauti na Fortune alisajiliwa na Sir Alex Ferguson miaka kadhaa nyuma lakini alikuwa mtu tofauti na wengine katika kikosi cha Manchester United cha kipindi kile aliishi maisha ya kifahari na yenye anasa ndani yake. Maisha aliyoishi Eric hayakuwa yanarandana na Sir Alex mwishowe aliuzwa sababu vitu alivyofanya nje ya uwanja alishindwa kuvihamishia ndani ya uwanja. Alipoteza uwezo ambao ulimfanya asajiliwe na timu ya ndoto zake Manchester United.

Tangu Eric aondoke United sijaona mchezaji mwingine kutoka Afrika akitinga uzi wa United zaidi ya Mame Diouf ambaye alitoka kwenye shule ya kukuzia vipaji. Sir Alex ana mengi moyoni kuhusu wachezaji wa Afrika nadhani mifano anayoweza kutoa ni Fortune na Djemba Djemba. Kitu kingine ambacho Sir Alex alichochukia kuhusu wachezaji wa Afrika ni michuano ya AFCON kufanyika wakati ligi kuu zinaendelea ilisababisha timu kuwa na mapengo ambayo kuzibwa ingekuwa kazi kubwa kama timu ingetegemea mchango zaidi wa wachezaji wa Afrika. Tunajaribu kuona Yaya Toure alivyokuwa anaiacha Manchester City katika wakati mgumu ndani ya mwezi mmoja. Sir Alex ana jambo kuhusu hili lakini ameamua kukaa kimya sasa,muda wake umeshapita.

Baada ya miaka mingi kupita Manchester United wamemsajili Eric Bailly. Ni mchezaji kutoka Ivory Coast. Ni Mwafrika kabisa. Lakini zama zimebadilika Bailly anaingia katika mikono ya mtu ambaye ana wahusudu wachezaji weusi. Eric anaingia kwenye mikono ya mtu ambaye anaijenga United mpya.

Katika timu ambazo Mourinho amepitia zote amefanya kazi na wachezaji kutoka Afrika. Porto alikuwa na Ben McCarthy. Chelsea aliwaleta Obi, Essien na Drogba. Inter Milan alikuwa na Eto’o,Mariga na Muntari. Real Madrid alikuwa na Essien na Adebayor na wengine wengi. Mourinho anaamini wachezaji kutoka Afrika wanatoka katika safari ndefu ya kutafuta mafanikio unapokuwa nao wana jaribu kuonesha thamani yao ili kuwa na mafanikio na mara nyingi ni mafanikio binafsi ya kifedha.

Eric Djemba Djemba alionyesha tabia halisi za Waafrika kama anavyofanya Adebayor, Eto’o na wengine katika matatuzi binafsi ya fedha. Kiuhalisia Eric Bailly anaingia katika mfano wa Fortune hana makuu japo huwa wanasema ukitaka kujua tabia halisi ya mwanaume basi mpe fedha.

Sitaki kuongelea umri wake wa kwenye passport sababu hakuna asiyejua wachezaji kutoka Afrika huwa wanapunguza umri. Kwa upande mwingine United itafanikiwa kibiashara zaidi katika soko la Afrika kwa kuwa Bailly atafungua milango ya United kuuza bidhaa zao hasa mauzo ya jezi.

Mbwembwe za Eric Djemba Djemba hazionekani kwa Eric Bailly. Bailly amekuja na roho ya Fortune yule aliyependwa na Sir Alex. Credit:Dauda
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top