Video: RONALDO ALIVYOWAZUIA ASKARI KUMKAMATA SHABIKI ALIYETAKA KUPIGA ‘SELFIE’

Licha ya machungu ya kushindwa kupata ushindi kwenye mchezo wa Ureno vs Austria, superstar wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo aliwazuia walinzi wa uwanja waliokuwa
wanataka kumwondosha shabiki aliyevamia uwanjani na kupiga naye selfie.

Baada ya mchezo kumalizika, ghafla shabiki alishuka toka jukwaani na kuvamia uwanjani kisha kumwelekea Ronaldo akitaka kupiga naye picha ‘selfie’. Walinzi wa uwanjani wakamkimbilia shabiki huyo na kutaka kumtoa uwanjani lakini Ronaldo aliwazuia kisha kupozi na shabiki huyo kwa ajili ya picha.

Wakati mashindano ya Euro yakiendelea, nchini Ufaransa kumekuwa na hali ya wasiwasi huenda matukio ya kigaidi yakatokea katika kipindi hiki. Ulinzi umekuwa ukiimarishwa kila kukicha lakini bado matatizo madogomadogo yamekuwa yakijitokeza.

Kila mtu amekuwa akifurahia hali ya utulivu ya sasa huku kukiwa hakujaripotiwa vurugu za mitaani pamoja na urushaji wa mafataki uwanjani, shabiki huyo alijitosa uwanjani na kuwaacha watazamaji wakisubiri kuona walinzi watachukua hatua gani.
Hii hapa video inayokupa fursa ya kushuhudia tukio zima

Magazeti ya leo jumapili june 19, 2016 bofya hapa

Vibonzo:Katuni tano bora zaidi leo Jumapili June 19, 2016 bofya hapa


HABARI KUU LEO BOFYA HAPA
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top