VARDY ATABAKI LEICESTER – WENGER


Kocha wa Arsenal Arsene Wenger anaamini kwamba Jamie Vardy hataikataa Arsenal na kubaki Leicester

Maneno haya yanakuja baada mmiliki wa Leicester Aiyawatt Srivaddhanaprabha kusema kwamba Vardy hatabaki na mabingwa hao wa England msimu ujao, Lakini mchezaji mwenyewe alipoulizwa alikataa kueleza atacheza wapi msimu ujao.

Alipoulizwa kwenye mkutano mbele ya mechi ya England dhidi ya Slovakia Euro 2016 Jumatatu Vardy alisema kwamba yeye anafikiria michuano ya Euro tu kwa hivi sasa na si kingine.

Wenger alipoulizwa kuhusu kumleta Vardy England alisema: “Hapana Jamie Vardy yuko Leicester kwa sasa hivi na kwa ninavyojua mimi, Jamie Vardy atabaki Leicester msimu ujao.”

The Gunners waliweza kutuma dau la Paundi million 22 wiki kadhaa zilizopita dau ambalo lilihakikisha kwamba Leicester hawana budi kukubali kutokana na kipengele kwenye mkataba wa Jamie Vardy. Lakini Vardy alichagua kutofanya maamuzi yeyote mpaka pale michuano ya Euro itapoisha ili aweze kutia jitihada zake zote kwenye timu ya England.

Vardy aliwekwa Benchi kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Russia ila aliweza kujipatia goli alipotokea benchi kwenye mechi ya pili dhidi ya Wales.
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top