SUALA LA KESSY KUCHEZA AU KUTOCHEZWA LAACHWA MIKONONI MWA YANGA

Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) limetoa ufafanuzi kuhusiana na beki wa Yanga, Hassan Kessy kuhusu mechi ya leo ya Kombe la Shirikisho kati ya Yanga dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria.

Awali, shirikisho hilo, lilieleza kuhusiana na suala la Kessy kulazimika kuwa na barua ya ruhusa kutoka Simba kwa kuwa ni klabu aliyotoka.

“Suala la kama hakuna malalamiko katika klabu anayotokea ni muhimu sana, baada ya hapo ni kuangalia kama usajili wa michuano hiyo umefuatwa. Kuna aina mbili, kwenye mtandao na kawaida.

“Kama Caf imetoa leseni, kunakuwa hakuna shida. Lakini kunaweza kuwa na angalizo la kuangalia kama mchezaji hana mkataba tena na klabu aliyotokea au walimalizana kwa kufuata taratibu zote.

“Kama atakuwa amemaliza mkataba na klabu aliyotokea, hakika hakuna tatizo hata kidogo na linaloangaliwa hapo ni hivi; usajili wa Caf umekamilika? Leseni imetoka? Kama hayo yametekelezwa, hakuna tatizo,” alisema.

Alipotafutwa mara ya pili kuhusiana na suala la Kessy, Binyam alisema: “Nimeambiwa Yanga wamezungumza na wenzetu wakati wa pre-match meeting kule Algeria, wameuliza maswali yote na kujibiwa vizuri na wameelewa.

“Ninaamini wachezaji wao watakuwa hawana tatizo kwa maana ya usajili wa Caf. Kwenye suala la usajili katika klabu walizotoka, hili tunaweza kusubiri chama cha nchi yenu (TFF) ndiyo waseme. Lakini hadi sasa, inaonekana wachezaji hao wanaweza kutumika, hilo tuwaachie wao (Yanga).”

Kwa kauli hiyo inaonekana Yanga, wana kila sababu ya kuwatumia Kessy, Juma Mahadhi, Adnrew Vicent ‘Dante’ na Beno Kakolanya ambao wamesajiliwa. Lakini Obey Chirwa raia wa Zambia atalazimika kusubiri wakati Yanga ikipambana kumtafutia usajili wake wa leseni kutoka Caf.

Lakini Msemaji wa Caf, Junior Binyam amesema kinachotakiwa kufuatwa katika hili ni Yanga kuangalia kama wamekamilisha taratibu za usajili za michuano ya Kombe la Shirikisho.

Credit: salehjembe

Magazeti ya leo jumapili june 19, 2016 bofya hapa

Vibonzo:Katuni tano bora zaidi leo Jumapili June 19, 2016 bofya hapa


HABARI KUU LEO BOFYA HAPA
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top