Scotland kuzuia Uingereza kuondoka EU



Waziri Kiongozi wa Uskochi, Nicola Sturgeon, anasema bunge la Scotland linaweza kupiga kura kuzuwia Uingereza kutoka katika Umoja wa
Ulaya.

Ali-iambia BBC anaamini, kikatiba, Uskochi lazima itoe idhini piya, kwamba Uingereza inaweza kumaliza uanachama wake katika EU na yeye atawasihi wabunge wa Scotland kutumia haki yao hiyo.

Uskochi ilipiga kura kwa wingi kubaki katika umoja huo

Bibi Sturgeon alisema, anataka kuwalinda watu wa Scotland na matokeo mabaya na ambayo yatawaumiza, nchi itapotoka katika Umoja wa Ulaya

Ameshazungumza juu ya uwezekano wa kufanya kura nyengine ya maoni, kujitenga na Uingereza.
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top