Ricardo Quaresma aipeleka Ureno robo fainali Euro


Ricardo Quaresma akishangilia baada ya kufunga bao 
Kwa ufupi

Lens, Ufaransa. Timu ya Ureno imeingia hatua ya robo fainali ya michuano ya Euro 2016 nchini Ufaransa baada ya kuichapa Croatia bao 1-0.


Kwa matokeo hayo, Ureno sasa itakumbana na Poland katika hatua ya robo fainali huku Wales chini ya nyota wake Gareth Bale wakisubiri wapinzani wao katika hatua hiyo.


Katika mechi hiyo iliyokuwa ya vuta nikuvute, safu ya ulinzi ya Croatia iliwazuia nyota Louis Nani na Cristiano Ronaldo wasifanye madhara langoni mwao huku Ivan Rakitic na Lukas Modric wakiichachafya vilivyo ngome ya Ureno pasipo mafanikio.


Hata hivyo, mpambano huo ulimalizika kwa suluhu ndani ya dakika 90.


Alikuwa ni straika Ricardo Quaresma katika dakika ya 117 aliyewanyanyua Wareno baada ya kufunga kwa kichwa mpira uliotemwa na kipa wa Croatia.


Kipa huyo alitema mpira uliopigwa na Cristiano Ronaldo aliyekuwa amewekwa chini ya ulinzi mkali na mabeki wa Croatia.


Mechi hiyo ilitanguliwa na nyingine mbili za Poland iliyoitoa Uswisi kwa jumla ya penalti 5-4 huku Wales chini ya nahodha wake Bale ikiifunga Ireland Kaskazini 1-0 na kuifanya timu hiyo kutinga hatua ya nane bora.


Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top