Prof. Makame Mbarawa Amteua Mhandisi Deusdedit Conatus Vitalis Kakoko kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
YAH: UTEUZI WA MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA
BANDARI TANZANIA (TPA)
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame M. Mbarawa, leo tarehe 25 Juni, 2016 amemteua Mhandisi Deusdedit Conatus Vitalis Kakoko kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania.


Mhandisi Kakoko amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Ephraim Mgawe ambae uteuzi wake ulitenguliwa.


Mhandisi Kakoko ni Meneja wa miradi kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).


Uteuzi huu unaanza mara moja.
Ramsey V. Kanyanga
KAIMU KATIBU WA WAZIRI
25/06/2016
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top