WALIMBWENDE JIJI LA ARUSHA WAAHIDI KUTOACHIA TAJI LA MISS TANZANIA 2016


Kusimamishwa kwa shindano la umrembo Tanzania (Miss Tanzania ) kwa mwaka mmoja imekuwa ni changamoto kubwa kwa waandaaji wa <endelea bofya kichwa cha habari hii juu>
shindano hilo, kwani warembo wengi wamesahau mambo kibao ndani ya mashindano hayo pia kueleza kuwa shindano hilo limepoteza umaarufu wake.

Hayo yamebainishwa na muaandaaji wa shindano la kumsaka mrembo wa mkoa wa Arusha kutoka katika kampuni ya Tour Visual Entertainment, Penda Simwita wakati akiongea na mwaandishi wa habari jana katika kambi ya kumuandaa Miss Arusha.

Alisema kuwa kwa upande wake shindano hilo limekuwa gumu kidogo, kwani warembo wengi walibweteka na kujisahau kuwa kuna shindano kama hili kwa mwaka huu, hivyo ilimlazimu kutembelea katika vyuo mbalimbali vya hapa mkoani Arusha kwa ajili ya kuwasaka warembo watakaoshiriki shindano hili.

"Pamoja na kuwatafuta,tumefaniwa kuwapata warembo wazuri wenye sifa na naamini wataweza kutetea taji la Miss Tanzania,kwani wana uwezo na kizuri zaidi najiamini naweza kuwaandaa maana hata mrembo ambaye anashikilia taji sasa hivi alitoka mkoa wa Arusha" alisema Mwandaaji huyo.

Mmoja wa warembo wanaoshiriki shindano hilo ,Maurine Ayubu alieleza hisia zake za kufurahi kushiriki shindano hilo,alisema kuwa ana uwezo wa kufanya vizuri,na kwamba ana uhakika wa kufanya vyema kwa sababu sifa zote za kuwa mrembo wa Mkoa wa Arusha anazo na kwamba anaamini atatetea taji la Miss Tanzania libaki Arusha kama linavyoshikiliwa kwa sasa na mrembo wa Tanzania Lilian kamazima 

Jumla ya warembo 17 kutoka katika mitaa mbalimbali na wilaya mkoani hapa wanatarajiwa kupanda jukwaani mapema May 28 mwaka huu katika ukumbi wa Hotel ya Naura Spring kwa ajili ya kumsaka mlibwende wa mkoa wa Arusha ambaye atawakilisha mkoa katika kinyang'anyiro cha kumsaka mrembo wa Tanzania na tukumbuke mpaka hivi sasa taji hilo la mrembo wa Tanzania linashikiliwa na mrembo kutoka mkoa wa Arusha Lilian Kamazima .
Baadhi ya warembo wanaoshiriki shindano la kumsaka mlibwende wa mkoa wa Arusha wakiwa katika pozi
warembo hao wakiwa wanacheza hii ikiwa ni moja ya mazoezi yao wanayoyafanya ndani ya ukumbi wa hoteli Naura Spring Arusha ambapo wameweka kambi


Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top