PICHA 7: YANGA WALIVYOWASILI MJINI BEJAIA KWA AJILI YA MECHI YA J’PILI

Wakitoka nje ya uwanja wa ndege wa Bejaia
Yanga tayari wameshatua kwenye mji wa Bejaia, Algeria kwa ajili ya mchezo wao wa kombe la shirikisho Afrika dhidi ya MO Bejaia.

Kikosi cha Yanga kimetinga Bejaia kikitokea moja kwa moja Uturuki, wamefika salama na kocha mkuu Hans van Pluijm amesema, wako tayari kwa mchezo na hawahofii wapinzani wao, watacheza mpira wao na kitu muhimu ni kupata matokeo.wakipanda basi kuondoa uwanja wa ndege wa Bejaia

Hakuna majeruhi lakini Yanga itamkosa Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ambaye anatumikia kadi nyekundu aliyoipata kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya GD Sagrada Esperanca.


Yanga walimtanguliza kiongozi wao Mohamed Nyenge ambaye alitafuta hotel pamoja na usafiri ingawa wenyeji walitakiwa kuwandaalia usafiri lakini Yanga walifanya hivyo kama tahadhari ambapo Bw. Nyenge alikodi basi kubwa kwa ajili ya kubeba wacheaji.Makocha wa Yanga Hans Pluijm na msaidizi wake Juma Mwambusi wakiwa na mkuu wa msafara wao haapa Mohamed Nyenge wakielekea hotel ya Raya waliyofikia

Uongozi wa MO Bejaia ulikuwa umewaandalia Yanga mabasi mawili madogo aina ya Coaster, wachezaji wa Yanga walipofika wakaingia moja kwa moja kwenye basi kubwa lililokodiwa na Nyenge, viongozi pamoja na makocha wakapanda kwenye mabasi madogo yaliyoandaliwa na timu ya MO Bejaia.Dante akishuka kwenye basi kuelekea hotelini

Yanga wamepanga kufanya mazoezi yao usiku huu majira ya saa 4:15 kwa saa za Algeria sawa na saa 6:15 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.Mwashiuya akishuka pia

Mchezo unatarajiwa kuchezwa siku ya Jumapili saa 4:15 usiku kwa saa za Algeria ambapo kwa Tanzania itakuwa ni saa 6:15 usiku.
Credit :dauda
HABARI KUU LEO  BOFYA HAPA
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top