Nape azindua msimu wa 6 wa michuano ya Airtel Rising Stars 2016



 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye leo Juni 26.2016 amezindua msimu wa sita (6) wa mashindano ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars, tukio lililofanyika
Makao makuu ya kampuni hiyo ya mtandao wa simu jijini Dar es Salaam.

Katika tukio hilo, mbali na Nape, pia Rais wa TFF, Jamali Malinzi naye aliungana pamoja na viongozi wengine na wadau wa soka. Awali Waziri Nape alipatiwa taarifa mbalimbali namna kampuni hiyo ilivyojikita katika kuinua vipaji vya vijana na michezo kwa ujumla ambapo kwa vijana waliopo sasa ambao ni chimbuko la program hiyo wameanza kua lulu kwa taifa hasa uwezo wao wa kisoka.

Akizungumza katrika tukio hilo Nape alieleza: “Program za soka za vijana ndiyo muhimili wa maendeleo ya soka popote pale duniani. Ndio maana nasisitiza umuhimu wa mashindano ya Airtel Rising Stars ambayo matunda yakek yameonnekana Dhahiri katika kipindi cha miaka mitano iliyopita” alisema Nape.

Nape pia aliipongeza Airtel kwa progamu hiyo kwani miongoni mwa wachezaji wa timu ya Taifa ya Vijana wa umri wa chini ya miaka 17, wanatoka katika program hiyo ya Airtel Rising Stars hivyo amewataka viongozi wanaosimamia soka hapa nchini kuisimamia vizuri program hiyo ya Airtel.

Alisema kushirikisha vijana hasa Wasichana na Wavulana ni jambo bora sana katika kukuza michezo hapa nchini hivyo ameiunga mkono na kuwapongeza kwani inasaidia Taifa katika kufikia malengo yake.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Bi. Beatrice Singano amemuakikishia Waziri Nape kuwa Airtel Tanzania ina nia thabiti ya kuendeleza kudhamini michuano hiyo ambayo imesaidia kuzalisha wachezaji wengi chipukizi hivyo kuendeleza mchezo huo maarufu hapa nchini.

Aidha, amebainisha kuwa,program hiyo hapa nchini inafanyika chini ya mwamvuli wa kampeni ya Airtel FURSA iliyozinduliwa mwaka jana kwa lengo la kuwahamasisha vijana kutumia fursa kupitia uwezo wa vipaji vyao hasa mpira wa miguu kuwa chanzo cha kipato chao.

“Kwa kuwa na wateja wengi nchi nzima Tanzania Bara na Zanzibar. Tunatakiwa kuendelea kutoa sehemu ya faida yetu kwa jamii kupitia mchezo wa mpira wa miguu ambayo ni maarufu hapa kwetu kuliko mchezo mwingine Hii ni njia ya kuwashukuru wateja wetu kwa kutuunga mkono” alieleza Bi Beatrice Singano.

Kwa upande wake, Rais wa TFF, Jamali Malinzi alipongeza program hiyo ya Airtel Rising Stars kwani imeleta mapinduzi na kubadilisha kabisa sura ya mchezo wa soka hapa nchini.

Airtel Rising Stars mwaka huu itashirikisha mikoa ya Mwanza, Morogoro, Mbeya, Temeke, Ilala (Wavulana) huku kwa mikoa itakayoshirikisha Wasichana ni pamoja na Ilala, Kinondoni, Temeke, Arusha, Lindi na Zanzibar.

Naye Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando ilieleza kuwa, Airtel itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuleta maendeleo ikiwemo kupitia programu zake mbalimbali ikiwemo hiyo ya soka.

“Tunajivunia mafanikio ya Airtel Rising Stars ambayo yametoa mchango mkubwa katika maendeleo ya mchezo wa soka nchini. Wachazeji kutoka programu hii ya Airtel Rising Stars hivi sasa wako katika timu za daraja la kwanza, ligi kuu Tanzania Bara na timu za taifa hasa ile ya U-20 na timu ya wanawake Twiga Stars,” alibainisha Mmbando mara baada ya uzinduzi huo.

Imeandaliwa na Andrew Chale,modewjiblog

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akipatiwa maelekezo ya moja ya vijana walioiburiwa na programu hyo ya Airtel Rising Stars ambaye pia wapo katika timu ya Taifa ya Vijana walio chini ya umri wa miaka 17.

Rais wa TFF, Jamali Malinzi akizungumza katika tukio hilo

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Bi. Beatrice Singano akizungumza katika uzinduzi huo..

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akizungumza katika uzinduzi huo

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akijiandaa kupiga mpira kuelekea golini kuashiria uzinduzi rasmi wa michuano hiyo..

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akipiga mpira kuelekea golini kuashiria uzinduzi rasmi wa michuano hiyo

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akifunga bao safi katika ufunguzi huo kuashiria uzinduzi rasmi wa michuano hiyo

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye katikati akipiga picha ya pamoja wakati wa uzinduzi huo. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akipata picha ya pamoja na maafisa wa Airtel Tanzania pamoja na viongozi wengine wa soka hapa nchini. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akipata picha ya pamoja na maafisa wa Airtel Tanzania pamoja na viongozi wengine wa soka hapa nchini. wakati wa tukio hilo la Airtel Rising Stars 2016.
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top