GRIEZMANN AIBEBA UFARANSA MGONGONI HADI ROBO FAINALI EURO 2016



Timu ya taifa ya Ufaransa ambao ndiyo wenyeji wa michuano ya Euro 2016 wametoka nyuma na kuifunga Jamhuri ya Ireland kisha kutinga hatua ya
robo fainali ya michuano hiyo.

Kikosi cha Ireland kilitangulia kupata bao na kuongoza kuanzia dakika ya pili baada ya Robbie Brady kupachika bao kwa mkwaju wa penati kufuatia Shane Long kufanyiwa madhambi kwenye eneo la hatari.

Lakini Ufaransa walikuja juu na kusawazisha bao hilo kupitia kwa Antoine Griezmann ambaye alifunga kwa kichwa kabla ya kuzamisha bao la pili na la ushindi la ushindi kwa wenyeji wa michuano hiyo.

Shane Duffy alitolewa nje kwa kadi nyekundu kutokana na kumchezea vibaya Griezmann na kuiacha timu yake ikicheza pungufu.

Kikosi cha Didier Deschamps kitapambana na England au Iceland kwenye hatua ijayo mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Stade de France Jumapili July 3.

Dondoo muhimu
Ufaransa ilitoka nyuma na kushinda mechi kwenye fainali za Euro kwa mara ya kwanza tangu ilipofanya hivyo mwaka 2004 dhidi ya England.
Griezmann ni mchezaji wa kwanza wa Ufaransa kufunga magoli matatu kwenye fainali za Ulanya ndani ya msimu mmoja tangu Zinedine Zidane mwaka 2004 (3).
Robbie Brady ni mchezaji wa kwanza wa Jamhuri ya Ireland kufunga mfululizo kwenye mechi ya mashindano ya Ulaya.
Jamhuri ya Ireland walifunga goli lao kutokana na shuti pekee lililolenga goli katika mchezo huo.
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top