Mkapa aunguruma: Tanzania inahitaji Mijadala ya wazi tena Makini, agusia Katiba iliyokwama (VIDEO)




Anasema kiongozi lazima asikilize. Hii nchi tutaiendeleza sisi wenyewe. Tuache kugombana bila Uchambuzi wa Kina. Ametolea mfano Mkwamo wa katiba, kasema ilitakiwa tuchambue na kutafakari Nini kiliikwamisha na nini kifanyike sio kulaumu tu.


Kasema ukiwa unaongea sana inabidi tutafakari jinsi ya kukudhibiti sababu saa nyingine mtu akiongea sana anakutoa kwenye njia na Malengo.


Asema nchi yetu Tanzania ndiyo yenye magazeti mengi, ingekuwa ndo kipimo basi sisi tumeendelea kweli kweli.


Mkapa amesema yeye ndie aliemuita Agha Khan aje aanzishe magazeti mengine hapa ndiyo yakaja mengine ya Mwananchi na the Citizen.


''Kwa mfano Prof Shivji amezungumzia kuhusu uhusiano wa kibiashara kati ya powerful block na nchi za Afrika, je ni uhusiano gani wa kibiashara utakaokuwepo kati ya wenye nguvu na wasio na nguvu?'' Alisema Mkapa


Amesema tunapenda kuzungumzia watu kuliko sera. Fuatilia michango ya wabunge Vijana Bungeni ambao wengine wanatoka hapa chuo kikuu, wana hoja gani? Wanazungumza nini?

Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top