Blatter atoboa siri ya upangaji wa michezo katika Mashindano ya Ulaya

Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Sepp Blatter amefunguka kuhusu upangaji wa mashindano ya Ulaya na kueleza kuwa kuna mchezo
ambao umekuwa ukifanyika wakati wa upangaji wa michezo hiyo.

Akifanya mahojiano na kituo cha La Nacion, Blatter ameeleza kumekuwepo na upangaji wa michezo kwa kutumia mipira ambayo inakuwa ndani ya kapu la kuchanganyia mipira na wanachokifanya ni anayekwenda kuchagua mpira anatumia mpira ambao unakuwa na joto au unakuwa na kawaida.


Kapu linalotumika kuweka mipira

“Ndiyo, nimeona kwa macho yangu ni kama usaliti … ni katika mashindano ya Ulaya. Unaweza kuona inatumika mipira kwa kuwa ya moto au ya baridi. Nina ushahidi wa hilo,

“Sijawahi kuchota sana mipira, marais wengine walifanya zaidi kwa kuchukua wao wenyewe mipira kutoka katika kikapu,” alisema Blatter.
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top