Maafisa
wa uchukuzi nchini Tanzania wanachunguza iwapo mabaki ya ndege
yaliyopatikana ufuoni ni ya ndege ya Malaysia iliyotoweka miaka
miwili iliyopita.
Picha za mabaki hayo yaliyopatikana visiwa vya Pemba zimekuwa zikisambaa sana mtandaoni.
Maafisa wa Tanzania wamewasiliana na maafisa wa Malaysia ambao wanapanga kutuma wachunguzi,
Hilo litawezekana tu wakati watengenezaji wa ndege hiyo watafika na kuchunguza mabaki hayo.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uchukuzi wa Ndege Tanzania Redemptus Bugomola ameambia BBC kwamba bado ni mapema mno kubaini iwapo mabaki hayo ni ya ndege ya MH370.
Shirika la habari nchini Malaysia Bernama lilimnukuu waziri uchukuzi nchini humo Liow Tiong Lai, akisema kuwa mabaki ya ndege hiyo yatafanyiwa uchunguzi kubainia ikiwa yana uhusiano na ndege ya Malaysia iliyopotea ya MH370.
"Mabaki hayo ya ndege ni makubwa ... lakini ni baada tu ya kubaini kwamba ni ya ndege aina ya Boeing 777 ndipo tutatuma wachunguzi huko kwenda kuchunguza iwapo kweli ni ya MH370 au la," amesema Liow.
Ndege hiyo ya Boeing 777 nambari MH370 ilitoweka 2014 ikiwa na watu 239 muda mfupi baada ya kupaa kutoka Kuala Lumpur ikielekea Beijing.
Vipande vya ndege hiyo vilipatikana katika visiwa vya Reunion Julai mwaka 2015.
Hivi majuzi, mabaki ya ndege sawa na hiyo yalipatikana Madagascar lakini baada ya uchunguzi ikabainishwa kwamba hayakuwa ya ndege hiyo ya MH370.

Habari zilizopo katika Magazeti ya Leo Jumatatu June 27, 2016 bofya hapa
Vibonzo:Katuni tano bora zaidi leo Jumatatu June 27, 2016 bofya hapa
Video: Rais Magufuli afanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya na kufanya mabadiliko kidogo ya wakuu wa Mikoa BOFYA HAPA
alert:Maombi Ya Mikopo Ya Wanafunzi Wa Elimu Ya Juu 2016/2017Bofya hapa
Breaking news: Rais Magufuli ateua Wakuu wa Wilaya na kufanya mabadiliko kidogo ya wakuu wa mikoa bofya hapa
Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA