GOLIKIPA WA UJERUMANI AJIUNGA NA WWE

Golikipa wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani na klabu ya Werder Bremen Tiem Wiese (kushoto) akitambulishwa rasmi ndani ya WWE

Golikipa wa zamani wa Ujerumani na klabu ya Werder Bremen Tiem Wiese ametangaza rasmi kujiunga na WWE na ataanza mazoezi katika kituo chao cha mazoezi hivi punde.

Wiese ilibidi ajiunge na WWE mwaka 2014 ila aliambiwa kwamba anahitaji muda na mazoezi zaidi kabla ya kuchaguliwa kujiunga na WWE.

Laakini Wiese alitangaza rasmi kukubali offer kutoka kwa Rais msaidizi wa masuala ya vipaji WWE Paul Levesque ama kwa jina lake maarufu la ‘Triple H’ ya kujiunga na kituo cha WWE Perfomance kilichopo huku Orlando Florida.

Akiongea na mtandao wa WWE Triple H alisema “Tim ni mkali sana sasa ni zamu yake kuonesha uwezo wake, mambo yakienda vizuri Florida atainga Dimbani.”

Kwa Upande wake ye Tim alisema “Nimejiandaa sana kwa ajili ya hili na nafurahi sana kupata fursa hii, nitafanya chochote kucheza WWE mwezi Novemba naitaka sana hiyo mechi.”

Tim Wiese aikuwa kipa hodari aliyefanikiwa kuchezea klabu kubwa ya Ujerumani ya Werder Bremen kwa miaka mingi, mwaka 2012 alijiunga na klabu ya TSG Hoffenheim kabla ya kustaafu mpira mwaka 2014 kwa sababu ya umri akiwa na miaka 34.

Tim Wiese alipata mafanikio makubwa katika mpira, alifanikiwa kuchaguliwa katika kikosi cha Ujerumani kilichoshiriki Kombe la Dunia mwaka 2010.
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top