EURO2016: NI VITA YA UFARANSA VS USWIZ, NANI KUONGOZA KUNDI A?

Michuano ya Euro inaendelea leo ambapo kundi A linahitimisha michezo yake, Ufaransa watakuwa na kibarua dhidi ya Uswizi wakati Albania watakuwa na kazi nzito mbele ya Romania. Hapa tunautupia macho mchezo wa Ufaransa na Uswizi, mchezo ambao endapo Ufaransa atapoteza basi Uswizi atashika hatamu ya kundi.

Mchezo huu utapigwa majira ya saa nne usiku kunako dimba la Stade Pierre-Mauroy lililopo manispaa ya Lille.

Katika mchezo wa leo, Ufaransa wanatarajia kuwarudisha kwenye kikosi cha kwanza nyota wao Paul Pogba na Antoine Griezmann kutokana na kiwango walichoonesha katika mchezo uliopita dhidi ya Albania.

Ufaransa wameshafuzu kuelekea hatua ya 16 bora lakini wanahitaji ushindi ama sare kuweza kujihakikishia nafasi ya kwanza katika kundi A.

Licha ya kuwa wenyeji wa michuano hii, Ufaransa wamekuwa wakipata ushindi wa tabu, mara nyingi wakisubiri mpaka dakika za mwisho kuweza kupata magoli ya ushindi, mfano mzuri ukiwa ni katika michezo yao ya awali dhidi ya Romania na Albania.

Uswizi kwa upande wao, wanahitaji ushindi kama si alama moja ili kuweza kufuzu kuelekea hatua ya 16 bora. Ushindi utawafanya kuongoza kundi wakati sare itawafanya kubaki nafasi ya pili na kufuzu moja kwa moja kulekekea hatua ya mtoano.

Taarifa muhimu za kila timu.

Uswizi wanaweza kuingia uwanjani bila kiungo wao maridadi Valon Behrami kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya goti.

Vile vile, mshambuliaji Haris Seferovic anaweza kotoanzishwa na nafasi yake kuchukuliwa na Breel Embolo ambaye ameonesha kiwango kizuri katika michuano hii.

Kwa upande wa Ufaransa, Paul Pogba na Antoine Griezmann wanatarajiwa kurudi kwenye kikosi cha kwanza huku Anthony Martial na Kingsley Coman wakipumzishwa kutokana na umuhimu wa mchezo.

Vile vile kiungo N’Golo Kante na straika Olivier Giroud wanaweza kupumzishwa kwa kuhofia kupata kadi nyingine za njano. Kila mmoja ana kadi ya njano, endapo wawili hawa wakicheza leo na kupata kadi, maana yake ni kwamba watakosa mchezo wa 16 bora. Sasa kutokana na umuhimu wao ni lazima kocha awapumzishe.

Kocha wa Uswizi Vladimir Petkovic anasema: “Kuna leo na kesho kwangu. Tutajitahidi kufanya kile liwezekananalo ili kupata matokeo. Sidhani kama matokeo tuliyopata kwenye kombe la dunia Brazil ya kufungwa mabao 5-2 yataathiri mchezo huu. Huu ni mchezo mwingine kabisa wenye morali mpya na malengo mapya.” “Bado hatujafuzu kwenda hatua ta mtoano hivyo tutajitahidi kupanga timu ya ushindi.”

Kwa upande wake, Didier Deschamps kocha wa Ufaransa anasema: [kuhusu suala la kutowaanzisha Pogba na Griezmann dhidi ya Albania], nadhani tulihitaji mawinga halisi katika mchezo ule. Paul anaweza kukupa vitu tofauti, lakini tulihitaji vitu tofauti zaidi. Pia kwa Griezmann, anaendelea vizuri kwa sasa, alicheza michezo mingi sana msimu ulioisha ndio maana nikampumzisha kidogo.

Rekodi zao katika mechi walizokutana.
Ufaransa na Uswizi wako kwenye kundi moja kwa mara ya nne katika michuano mikubwa saba iliyopita (Euro 2004, Kombe la Dunia 2006 na 2014, Euro 2016).
Ufaransa hawajafungwa na Uswizi katika mechi zao tatu za mwisho walizokutana katika michuano mbalimbali, wakiwafunga Euro mwaka 2014 na Kombe la Dunia mwaka 2014 na kutoka sare Kombe la Dunia mwaka 2006.
Ushindi wa mwisho wa Uswizi dhidi ya Ufaransa ulikuwa ni May 1992 (ushindi wa 2-1 mjini Lausanne). Tangu hapo hawajawahi kushinda tena katika michezo yao sita ya mwisho waliyokutana.
Mchezo wao wa mwisho waliokutana ulitoa magoli 7. Ilikuwa ni katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 aambapo Ufaransa walishinda 5-2. Hii ni zaidi ya michezo yao minne kabla ya hapo ambayo ilitoa jumla ya magoli sita

Uswizi
Uswizi hawajawahi kufuzu kuelekea hatua ya mtoano tangu waanze kushiriki michuano hii.
Magoli yote ya Uswizi mpaka sasa yametokana na mipira ya kona.
Magoli manne kati ya saba waliyopata kwenye michuano hii yametokana na mipira ya kutenga (set-pieces)……(penati mbili na kona mbili).
Katika mchezo dhidi ya Romania, Uswizi walifanikiwa kupiga mashuti 19, mashuti mengi zaidi kuwahi kupiga katika historia ya ushiriki wao.

Ufaransa
Hii ni mara ya tatu kwa Ufaransa kushinda michezo yao miwili ya awali katika michuano hii (mwaka 1984, 2000 na 2016).
Mpaka sasa Ufaransa hawajapiga shuti hata moja lililolenga langoni mwa timu pinzani kabla ya muda wa mapumziko.
Magoli tisa kati ya 10 ya Ufaransa katika michuano ya Euro, yamefungwa baada ya kipindi cha kwanza.
Ufaransa wameshinda michezo yao saba iliyopita ya michuano ya Euro waliyocheza katika ardhi ya nyumbani (mitano mwaka 1984 na miwili mwaka 2016).

Magazeti ya leo jumapili june 19, 2016 bofya hapa

Vibonzo:Katuni tano bora zaidi leo Jumapili June 19, 2016 bofya hapa


HABARI KUU LEO BOFYA HAPA
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top