Aliyewahi kuwa Makamu wa Rais Bemba ahukumiwa miaka 18 jela na ICC

Aliyekuwa kiongozi wa waasi nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Congo Jean-Pierre Bemba, amehukumiwa kifungo cha miaka 18 jela kufuatia uamuzi wa mahakama ya kimataifa ICC, kutokana na uhalifu wa kivita na unyanyasaji wa kingono.

Bemba alipatikana na hatia mwezi Machi kwa makosa ya uhalifu, uliotokea katika nchi jirani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, kati ya mwaka 2002 na 2003.
 Wafuasi wa Bemba wakifutilia hukumu kutoka DRC

Analaumiwa kwa kushindwa kuwazuia waasi wake wasiwaue na kuwabaka watu. Mawakili wa Bemba tayari wamesema kuwa watakataa faa kupinga hukumu hiyo.

Akitoa hukumu hiyo jaji Sylvia Steiner, alisema kuwa Bemba alishindwa kudhibiti waasi wake ambao walitumwa kwenda Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Bemba alikuwa ametuma zaidi ya wapiganaji 1,000 kwenda nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, kumsaidia rais wa zamani Ange Felix Patasse, kukubiliana na jaribio la mapinduzi.
Jean Pierre Bemba
Makamu wa rais wa zamani DR Congo
18
Miaka ambayo amefungwa jela na ICC
2002-2003 Kipindi ambacho anadaiwa kutekeleza uhalifu CAR
2008 Mwaka aliokamatwa Brussels
EPA 
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top