Aliyeibuka wa kwanza katika mtihani India afungwa jela

Mwanafunzi mmoja wa India amehukumiwa kifungo jela kwa kudanganya katika mtihani baada ya kujaribiwa kwa mara ya pili
.

Ruby Rai mwenye umri wa miaka 17 ambaye alikuwa wa kwanza katika mtihani huo katika jimbo la Bihar, alisema katika mahojiano kwamba somo alipendelo la sayansi ya siasa linahusu mapishi.

Baada ya kanda hiyo kusambaa ,bi Rai alilazimika kukalia tena mtihani na alikamatwa aliposhindwa huku matokeo yake ya mtihani yakifutiliwa mbali.

Aliwasilishwa mahakamani siku ya Jumapili ambapo hakimu alimuhukumu kifungo jela hadi tarehe 8 mwezi Julai.

Uamuzi wa kumpeleka jela umekosolewa kwa kuwa ni mtoto na kwamba badala yake angepelekwa katika jela ya watoto. Udanganyifu katika mtihani India

Gazeti la Hindu lilimnukuu afisa mkuu wa polisi Manu Maharaj akisema kuwa bi Rai atalazimika kubaini kwamba yeye ni mtoto.

Wakati huohuo agizo la kukamtwa limetolewa kwa wanafunzi wengine ambao walifanya vyema katika mtihani akiwemo Sauragh Shrestha ambaye alikuwa wa kwanza katika somo la sayansi lakini ambaye baadaye alishindwa kusema kwamba H20 ni maji.



Uingereza yatolewa michuano ya EURO 2016 Bofya hapa




News alert: Chile yatwaa Ubingwa tena Copa America Bofya hapa
Video: MESSI AKOSA PENATI NA KUISHUHUDIA CHILE IKITWAA UBINGWA COPA AMERICA bofya hapa 


Breaking news: Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameteua wakuu wa wilaya 139, na amefanya mabadiliko madogo ya wakuu wa mikoa Bofya hapa







Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA

HABARI KUU LEO BOFYA HAPA
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top