Iraq yatangaza vita vya kukomboa Fallujah

Wapiganaji wa IS wamedhibiti mji wa Fallujah kwa miaka miwili

Waziri Mkuu wa Iraq Haider al-Abadi ametangaza operesheni kubwa ya kijeshi ya kuukomboa mji wa <endelea bofya kichwa cha habari hii juu>Fallujah kutoka kwa wapiganaji wa Islamic State.

Kundi hilo liliuteka mji huo miaka miwili iliyopita.

Akiwa ameandamana na maafisa wakuu wa jeshi, Bw al-Abadi alitoa tangazo hilo moja kwa moja kupitia televisheni na kusema bendera ya Iraq karibuni itapepea katika mji wa Falluja.

Mji huo unapatikana takjriban kilomita 50 magharibi mwa mji wa Baghdad.AFP

Wanajeshi na polisi zaidi wametumwa kuuzingira mji huo.

Maafisa wa serikali awali walikuwa wamewatahadharisha maelfu ya raia ambao bado wamo katika mji huo, wengi wao jamaa za wapiganaji wa IS, kuuhama mji huo.

Licha ya kukabiliwa vikali, wapiganaji wa IS bado hudhibiti maeneo makubwa kaskazini na magharibi mwa Iraq, ukiwemo mji wa pili kwa ukubwa nchini humo wa Mosul.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top