KIKOSI cha timu ya Yanga kimefanya mazoezi yake ya mwisho katika uwanja wa Sagrada Esperanca Kwa ajili ya mchezo wao wa marudiano wa kombe la <endelea bofya kichwa cha habari hii juu>Shirishiko barani Afrika dhidi ya GD Sagrada Esperanca nchini Angola.
Yanga imewasili salama mjini Dundo, Angola jana jioni baada ya safari ya kutwa nzima huku wachezaji wakionekana kupata usumbufu wa kubadilisha usafiri pamoja na baadhi yao kupoteza mabegi.
Meneja wa timu Hafidhi Saleh amesema kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa kesho dhidi ya wenyeji ambapo anajua mchezo huo utakuwa mgumu sana kwao.
Amesema, wachezaji wamefanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya maandalizi ya kesho ila asubuhi watafanya mazoezi ya mepesi mepesi.
"Wachezaji wote wamefanya mazoezi ya mwisho lakini kesho asubuhi watafanya yale mepesi mepesi kuelekea mchezo wa kesho ambao ni muhimu sana kwetu,"amesema Saleh.
Saleh amesema, wanatarajia kesho watahakikisha wanapafa ushindi hasa baada ya wachezaji wao wawili ambao hawakucheza kwenye mechi ya Jijini Dar es salaam watakuwemo kwa ajili ya kuongeza nguvu.
"Ngoma na Kamosoku wamejumuika katika kuelekea mchezo huu hasa baada ya ule wa awali kuwepo jukwaani wakiwa wanatumikia adhabu ya kadi za njano walizozipata kwenye mchezo wa Al Ahly,"amesema Saleh.
Saleh amesema hali za wachezaji wote zipo vizuri na wamejiandaa kuweza kushinda mchezo huo ambao ni muhimu sana kwao na kama watafanikiwa kushinda basi watasonga mpaka hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho Afrika.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)