Paul Makonda ameanzisha mkakati wa kuokoa Ubadhirifu.


Mkuu wa Mkoa wa dsm Paul Makonda ameanzisha mkakati wa kuokoa Ubadhirifu unaofanywa na baadhi ya watumishi wa Serikali baada ya kubaini kuwa magari mengi yanatelekezwa na baadae kuuzwa kwa <endelea bofya kichwa cha habari hii juu>bei ya chini kwa baadhi ya watumishi kwa madai kuwa ni mabovu yaliyoshindikana kutengenezwa.

Akizungumza wakati wa zoezi la kuondoa magari manane ya Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa dsm ambayo yanadaiwa kukaakwa muda mrefu kwenye gereji kwa madai kuwa mabovu ambayo yangehitaji fedha nyingi kuyatengeneza Bw,Makonda amesema kuna watumishi ambao sio waadilifu wanaotumia mwanya huo kujiuzia magari kwa bei ya kutupa.

Amesema Mafundi Magari kutoka Tegeta wameamua kuchukua magari hayo na kuyatengeneza bure ikiwa ni mchango wao katika kuisaidia serikali ya awamu ya tano kukidhi mahitaji ya jamii.

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa DSM amewataka wananchi,Taasisi pamoja na Makampuni kuendelea kujitokeza katika Kampeni ya Kuchangia madawati kwa ajili ya wanafunzi wa Shule za msingi na Sekondari inayosimamiwa na Kituo cha chanel ten na Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa dsm ili kufikia upatikanaji wa madawati laki moja yanayohitajika.

Tayari mafundi hao wa magereji wa Tegeta wamechanga na kutengeneza madawati 100 baada ya kusikia matangazo ya Uchangiaji madawati kupitia kituo hiki cha chanel ten

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top