Alama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa imetoa wito kwa taasisi za serikali kuhakikisha zinatumia alama za jumuiya ya<endelea bofya kichwa cha habari hii juu> Afrika Mashariki (EAC) ambazo ni Bendera na wimbo wa jumuiya hiyo, kwenye ofisi zake sambabamba na alama za Taifa ikiwemo Bendera ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wimbo wa Taifa.
Hatua hiyo ni utekelezaji wa mkataba wa uanzishwaji wa jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo kifungu cha 7(a) kinasisitiza jumuiya hiyo kuwa ni ya watu, hivyo wananchi wa Tanzania watahusishwa katika hatua zote za mtangamano na kushirikishwa kikamilifu katika hatua mbalimbali za ustawi wa jumuiya ili kuijua kwa madhumuni pamoja na kunufaika na fursa mbalimbali zinazopatikana katika jumuiya hiyo.
Rai hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kikanda na kimataifa Mindi Kasiga, wakati alipozungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema wizara hiyo itaratibu zoezi la upatikanaji wa sampuli za alama hizo za jumuiya kwa gharama za taasisi husika.
Wakati huo huo, Mindi amesema Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa, ataongoza mazungumzo kuhusu mgogoro wa Burundi yanayotarajiwa kuanza Mei 21 hadi 24 jijini Arusha.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)