Waziri ataka wanaozaa kuongezwa ruzuku

Waziri anapendekeza ruzuku ya dola 90 kwa kila mtoto kila mwezi kuongezwa maradufu.

Waziri wa afya wa Italia, Beatrice Lorenzin, amependekeza kuzidisha mara dufu, ruzuku wanayopewa wazazi wanapopata mtoto, ili kuwafanya watu wazae zaidi.

Akihojiwa na gazeti la La Repubblica, Bi Lorenzin alisema, ikiwa mtindo wa sasa utaendelea, basi baada ya miaka 10, idadi ya watoto wanaozaliwa nchini Italia itapungua kwa asilimia 40 ikilinganishwa na mwaka 2010.

Alionya kuwa kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu wazee na wale wagonjwa nchi itakuja kuwa isiyojiweza.

Hivi sasa mzazi anapata ruzuku ya dola 90 kwa mwezi kwa kila mtoto akipendekeza kuwa ruzuku hiyo itaongezwa maradufu kwa familia zenye kipato cha chini na wastani.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top