Wapigwa vibaya na Wakala misitu baada ya Kuingia hifadhini


WATU watatu wamepigwa na kuumizwa vibaya sehemu mbalimbali za miili yao na maafisa wa wakala wa misitu Tanzania wa wilaya ya<endelea bofya kichwa cha habari hii juu> Geita (TFS) huku mtoto Getruda Cosimas 16 akijeruhiwa vibaya mikono yake yote kwa kile kinachodaiwa kuingia hifadhini bila kibali.

Tukio hili la kusikitisha limetokea May 13 mwaka huu majira saa saba mchana katika pori la Chibingo lililoko kata ya Nyamigota wilaya na Mkoa wa Geita.

Wakizungumza na Channel Ten ndugu zake pamoja na mashuhuda wamesema kuwa mtoto wao alikwenda kuokota kuni lakini walishangaa kupigiwa simu na wasamalia wema kwamba mtoto wao amepigwa na maafisa misitu na kutupwa kutelekezwa polini na hapa wanaeleza.

Diwani kata ya Rudete pamoja na mwenyekiti wa mtaa huo wamelaani kitendo walichofanyiwa wananchi huku wakiomba vyombo vinavyousika kuchukua hatu kwa waliofanya .

Pamoja na kwamba majeruhi watatu ambao hawakutambulika majina yao mara moja kwenda katika kituo cha polisi Katoro na kupewa PF3 NO KTR /RB/890/2016. ili wakatibiwe katika kituo cha afya Katoro walikolazwa siku tatu, cha kushangaza kaimu mganga mkuu Kilunga P. Kilunga amesema yeye hajui lolote huku meneja misitu Wilaya ya Geita Shadrack Msila akijitetea.

Jeshi la polisi Mkoani Geita limedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba faili limefunguliwa ili kubaini waliofanya kitendo hicho.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top