Wakuu wa mashtaka wataka Bemba apewe hukumu ndefu

Bemba alishindwa kuwazua waasi wake waliokuwa wakiwaua na kuwabaka watu katika taifa jirani la Jamhuri ya <endelea bofya kichwa cha habari hii juu>Afrika ya Kati.

Waendesha mashtaka kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita wametaka aliyekuwa makamu wa rais nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Jean Pierre-Bemba, kuhukumiwa kifungo kisichopungua miaka 25 jela baada ya kupatikana na hatia ya kushuriki kwenye uhalifu wa kivita mjini Hague.

Bemba mwenye umri wa miaka 53 alipatikana na hatia mwezi Machi, kwa kushindwa kuwazua waasi wake waliokuwa wakiwaua na kuwabaka watu katika taifa jirani la Jamhuri ya Afrika ya Kati mwaka 2002 na 2003.Hii ndiyo mara ya kwanza mahakama ya ICC imeliangazia suala la ubakaji kuwa silaha ya vita.

Alikuwa amewatuma zaidi ya wapiganaji 1000 kusaidia kuzima jaribio la mapinduzi.

Hii ndiyo mara ya kwanza mahakama ya ICC imeliangazia suala la ubakaji kuwa silaha ya vita, na mara ya kwanza mshukiwa amepatikana na hatia ya uhalifu uliofanywa na watu wengine waliokuwa chini ya uongozi wake.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top