Mashabiki wa Liverpool waonywa Uswizi

Mashabiki wa Liverpool

Zikiwa zimesalia Saa chache kabla ya fainali ya kombe la Europa League kati ya Liverpool na Sevilla, polisi mjini Basel, Uswizi wametoa onyo kutowaruhusu mashabiki wa <endelea bofya kichwa cha habari hii juu>Liverpool wasiokuwa na tiketi kuingia au kukaribia uwanja wa St Jakob-Park. Takriban mashabiki laki moja wanatarajiwa kufika nchini humo kuiandama timu yao ya The Reds wakisaka ubingwa wa bara Ulaya.

"Idadi tunayotarajia ni kati ya elfu 30 hadi elfu arobaini, lakini ni vigumu kutaja idadi kamili, mkuu wa polisi nchini Uswizi, Andreas Knuchel aliiambia BBC.

Knuchel ameongeza kuwa, wako tayari kuwapokea mashabiki wa Liverpool na kuwapa mazingira mazuri ya kusherekea.

"Kama huna tiketi ya kutazama mechi, usikaribie uwanja kwa sababu kuna sehemu za ukaguzi na hutoruhusiwa kuingia uwanjani. "

"Hoteli zote hazina nafasi, kama unasaka sehemu ya malazi, hautafanikiwa, utasubiri hadi asubuhi utakapoabiri ndege’’, alisema.

Hata hivyo, licha ya tahadhari, polisi wamesema kuwa watakabiliana na mashabiki kwa utulivu bila vurugu.

Baada ya ushindi wake dhidi ya Villareal, Kocha Jurgenn Klopp, aliwahimiza mashabiki wasiokuwa na tiketi kuandamana nao. Lakini sasa Klopp amewarai mashabiki wasalie makwao, msimamo unaougwa mkono na polisi wa Liverpool.

Kulingana na polisi wa Uswizi, ndege nane zaidi zimekodishwa ili kuwasafirisha mashabiki wa Liverpool kutoka Uingereza hadi Uswizi.

Shirikisho la soka barani Ulaya, UEFA limeshinikizwa kwa kuandaa fainali katika uwanja mdogo ulio na uwezo wa kuwalaki mashabiki 35,000 pekee.

Wafuasi wa Liverpool wametengewa nafasi elfu kumi pekee.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top